Roho
ni
umbile
la pekee lisiloonekana ambalo linasadikiwa kuwemo pamoja na
mwili
katika
binadamu
na kuunda hasa
malaika
(ambao kati yao wale wabaya wanaitwa ma
shetani
).
Katika
lugha
mbalimbali umbile hilo linafananishwa na
upepo
au
pumzi
.
Mungu
mwenyewe anasadikiwa kuwa roho bora. Kwa namna ya pekee
Ukristo
unasadiki moja ya
nafsi
za Kimungu ndani ya
Utatu
inayoitwa
Roho Mtakatifu
.
Pengine roho inafikiriwa kueleza tofauti kubwa mno ambayo inajitokeza kati ya binadamu na
sokwe
na
wanyama
wengine wote upande wa
akili
na
utendaji
, na ambayo haielezwi vya kutosha na tofauti katika
DNA
zao.
Inasadikiwa kuwa roho ndiyo sehemu bora zaidi ya mwanadamu na husadikiwa kuwa haifi bali hudumu
milele
. Roho humuunganisha mtu na
ulimwengu
wa kiroho ambao aghalabu huwa ni ulimwengu usioonekana na
macho
ya kawaida, yaani ya mwili.
|
Makala hii kuhusu mambo ya dini bado ni
mbegu
.
Je, unajua kitu kuhusu mada hii kama historia yake au uenezi wake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa
kuihariri na kuongeza habari
.
|