Alfred Nobel ( 21 Oktoba 1833 ? 10 Desemba 1896 ) alikuwa mhandisi na mwenye viwanda wa nchi ya Sweden .
Mwaka wa 1867 aligundua jinsi ya kutengeneza baruti kali. Pia aliboresha utoneshaji wa mafuta . Akafaulu kiuchumi akawa tajiri na wakati uleule mwenye wasiwasi kuhusu matumizi ya baruti aliyogundua kwa sababu aliona matumizi mabaya kwa ajili ya silaha . Hivyo katika hati yake ya wasia alianzisha Tuzo ya Nobel kwa ajili ya mafanikio ya kisayansi lakini pia kwa ajili ya amani duniani .
Kuanzia ilipoanzishwa tuzo ya Nobel watu mbalimbali wametunukiwa tuzo hiyo kama vile Albert Einstein , Niels Bohr , Max Planck , Mama Teresa , Nelson Mandela n.k.